Al-Hajj 22:8
الحجوَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَـٰدِلُ فِى ٱللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَـٰبٍ مُّنِيرٍ
Na katika watu wapo wanaobishana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu, wala uongofu, wala Kitabu chenye nuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya ilimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye nuru. [8]
[8] Na juu ya yaliyo tangulia bado wapo baadhi ya watu wanao jadili juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu, na wanakanya kufufuka bila ya msingi wowote wa ki-ilimu, wala uwongozi wa kweli, au Kitabu kilicho toka kwa Mwenyezi Mungu cha kumwonyesha. Basi ubishi wake ni wa pumbao na inda tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Miongoni mwa makafiri kuna wenye kujadili kwa njia ya ubatilifu kuhusu Allah Mtukufu, na kuhusu kumpwekesha Yeye, na kuhusu kumteua kwake mtume wake, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na kuhusu kuteremsha Kwake Qur’ani. Kujadili huko ni bila ya ujuzi, ufafanuzi wala kitabu kitokacho kwa Allah Mtukufu chenye ushahidi na hoja iliyo wazi,
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net