Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 9

Al-Hajj 22:9

الحج

ثَانِىَ عِطْفِهِۦ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۖ لَهُۥ فِى ٱلدُّنْيَا خِزْىٌ ۖ وَنُذِيقُهُۥ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ عَذَابَ ٱلْحَرِيقِ

Maana

Anayegeuza shingo yake ili kupoteza watu waiache njia ya Mwenyezi Mungu. Duniani atapata hizaya, na Siku ya Kiyama tutamwonjesha adhabu ya kuunguza.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Anaye geuza shingo yake ili kupoteza watu waache Njia ya Mwenyezi Mungu. Duniani atapata hizaya, na Siku ya Kiyama tutamwonjesha adhabu ya kuungua. [9]

[9] Na pamoja na hayo hugeuka upande kwa kiburi na kukataa kuikubali Haki. Na watu wa namna hii itakuja wapata hizaya na udhalili duniani kwa ushindi wa Neno la Haki, na Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa Moto wa kuunguza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hali akiipotoa shingo yake kwa kiburi na akiupa mgongo ukweli, ili awazuie wengine wasiingie kwenye Dini ya Allah Mtukufu. Basi huyo atapata udhalili ulimwenguni kwa kuangamia na mambo yao kufedheheka na Siku ya Kiyama tutamchoma kwa Moto.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net