Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 10

Al-Hajj 22:10

الحج

ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ يَدَاكَ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَيْسَ بِظَلَّـٰمٍ لِّلْعَبِيدِ

Maana

(Ataambiwa): Hayo ni kwa sababu ya yale iliyoyatanguliza mikono yako. Na hakika Mwenyezi Mungu si dhalimu kwa waja.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Ataambiwa): Hayo ni kwa sababu ya iliyo tanguliza mikono yako. Na hakika Mwenyezi Mungu si dhaalimu kwa waja. [10]

[10] Na ataambiwa: Hayo unayo yapata ya hizaya na adhabu ni kwa sababu ya uzushi wako na kiburi chako; kwani hakika Mwenyezi Mungu ni Muadilifu, hadhulumu. Wala hawaweki sawa Muumini na kafiri, na mwema na muovu; bali kila mmoja wao atamlipa kwa mujibu wa vitendo vyake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ataambiwa, «Adhabu hiyo ni kwa sababu ya maasia uliyoyafanya na makosa uliyoyachuma, na Allah Mtukufu Hamuadhibu yoyote pasi na dhambi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net