Al-Hajj 22:11
الحجوَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَعْبُدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ حَرْفٍ ۖ فَإِنْ أَصَابَهُۥ خَيْرٌ ٱطْمَأَنَّ بِهِۦ ۖ وَإِنْ أَصَابَتْهُ فِتْنَةٌ ٱنقَلَبَ عَلَىٰ وَجْهِهِۦ خَسِرَ ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْخُسْرَانُ ٱلْمُبِينُ
Na katika watu wapo wanaomuabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia heri, hutulia kwayo. Na ukimfikia msukosuko, hugeuza uso wake. Amehasiri dunia na Akhera. Hiyo ndiyo hasara iliyo wazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika watu wapo wanao muabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na Akhera; hiyo ndiyo khasara iliyo wazi. [11]
[11] Na miongoni mwa watu wapo wa namna ya tatu, ambao Imani bado haijatulia katika nyoyo zao, bali itikadi yao inayumba yumba. Maslaha ya nafsi zao ndiyo yanatawala katika Imani yao. Wakipata kheri hufurahi na hutulizana. Na wakipata shida yoyote katika nafsi zao, au mali zao, au wana wao, hurejea ukafirini. Hao huwa wamekosa duniani raha ya utulivu kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na nusura yake, kama Akhera walivyo kosa neema ambayo Mwenyezi Mungu amewaahidi Waumini walio thibiti na wakasubiri. Hiyo khasara ya mara mbili ndiyo khasara ya kweli kweli iliyo wazi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Miongoni mwa watu kuna anayeingia kwenye Uislamu kwa udhaifu na shaka, akawa anamuabudu Allah Mtukufu juu ya shaka na ukosefu wa uamuzi, ni kama yule anayesimama kwenye ukingo wa jabali au ukuta, hawi thabiti katika kusimama kwake, huifungamanisha Imani yake na ulimwengu wake: akiishi katika hali ya afya na ukunjufu huendelea kwenye ibada yake, na akipatwa na mitihani ya tabu na shida huyanasibisha hayo na Dini yake, na kwa hivyo huiacha. Ni kama yule anayegeuka kwa uso wake baada ya kulingana sawa, akapata hasara ya ulimwengu, kwani kukufuru kwake hakugeuzi chochote alichokadiriwa katika ulimwengu wake, akapata hasara ya Akhera kwa kuingia Motoni, na hiyo ni hasara inayoonekana waziwazi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net