Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 12

Al-Hajj 22:12

الحج

يَدْعُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُۥ وَمَا لَا يَنفَعُهُۥ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلضَّلَـٰلُ ٱلْبَعِيدُ

Maana

Badala ya Mwenyezi Mungu, yeye huomba kisichomdhuru wala kumnufaisha. Huko ndiko kupotea kwa mbali!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Badala ya Mwenyezi Mungu, yeye huomba kisicho mdhuru wala kumnufaisha. Huko ndiko kupotolea mbali! [12]

[12] Mwenye kukhasiri hivi humuacha Mwenyezi Mungu na akayaabudu masanamu yasiyo weza kumdhuru pindi akito yaabudu, wala hayamfai kitu pindi akiyaabudu. Kitendo chake huyo ndio kupotelea mbali na haki na uwongofu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Huyo aliyepata hasara anakiabudu kitu, badala ya Allah Mtukufu, kisichomdhuru kama akikiwacha, wala kumnufaisha kama akikiabudu. Huko ndiko kupotea kulioko mbali na haki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net