Al-Hajj 22:35
الحجٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَٱلصَّـٰبِرِينَ عَلَىٰ مَآ أَصَابَهُمْ وَٱلْمُقِيمِى ٱلصَّلَوٰةِ وَمِمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ يُنفِقُونَ
Wale ambao, anapotajwa Mwenyezi Mungu, nyoyo zao hutetemeka, na wanavumilia kwa yanayowasibu, na wanashika Sala, na wanatoa katika tulivyowaruzuku.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ambao, anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hutetemeka, na wanao vumilia kwa yanao wasibu, na wanao shika Swala, na wanatoa katika tulivyo waruzuku. [35]
[35] Wale ambao akitajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hupapatika kwa kumkhofu, na hunyenyekea kwa kutajwa kwake, na ambao wanasubiri kwa masaibu ya karaha na shida yanayo wapata kwa kujisalimisha mbele ya amri yake na hukumu yake, na wakashika Swala kwa ukamilifu wake, na wakatoa baadhi ya mali aliyo waruzuku Mwenyezi Mungu katika njia za kheri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanyenyekevu hawa wenye kujinyongesha (kwa Allah Mtukufu) miongoni mwa sifa zao ni kwamba wao Atajwapo Allah Mtukufu Peke Yake, wanaiogopa adhabu Yake na wanakuwa na hadhari wasimuasi, na wakipatikana na shida na matatizo, wanasubiri juu ya hayo wakiwa na matumaini kupata malipo mema kutoka kwa Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka, wanatekeleza Swala kikamilifu, na wao pamoja na hayo wanatoa, katika kile Alichowaruzuku Allah Mtukufu, katika mambo yanayowapasa ya Zaka, matumizi ya watoto na kila ambaye matumizi yake yanawalazimu, katika njia ya Allah Mtukufu na katika matumizi yanayopendekezwa yasio ya lazima.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net