Al-Hajj 22:34
الحجوَلِكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا لِّيَذْكُرُوا۟ ٱسْمَ ٱللَّهِ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّنۢ بَهِيمَةِ ٱلْأَنْعَـٰمِ ۗ فَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ فَلَهُۥٓ أَسْلِمُوا۟ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُخْبِتِينَ
Na kila umma tumewafanyia mahali pa kuchinjia mihanga ya ibada ili walitaje jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile walivyoruzukiwa katika wanyama wa mifugo. Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Kwa hivyo, jisalimisheni kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kila umma tumewafanyia mahala pa kuchinjia mihanga ya ibada ili walitaje jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile walivyo ruzukiwa katika wanyama wa mifugo. Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Jisalimishieni kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu. [34]
[34] Hizi faridha za Hija hazikukhusuni nyinyi peke yenu. Kwani tumewajaalia jamaa wote walio amini mambo ya kuwakaribisha kwa Mwenyezi Mungu, na wanataja jina lake, na wanamtukuza wakati wanapo chinja kwa kumshukuru kwa neema aliyo waneemesha, na kuwasahilishia wanyama wa mifugo, nao ni ngamia, ng'ombe, mbuzi na kondoo. Na Mwenyezi Mungu aliye kuwekeeni sharia nyinyi na wao ni Mungu Mmoja. Basi yasalimisheni mambo yenu yote kwake Yeye peke yake. Na vitendo vyenu visafisheni kwake, wala msimshirikishe na yeyote. Na ewe Nabii! Wape bishara ya Pepo na thawabu nyingi wale walio safisha niya zao kwa Mwenyezi Mungu na wakawa wanamnyenyekea Yeye miongoni mwa waja wake,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kila kundi lenye kuamini lililotangulia, tumelifanyia mambo ya ibada ya kuchinja na kumwaga damu, hayo ni kwa ajili wapate kutaja jina la Allah Mtukufu Aliyetukuka wakati wa kuchinja kile tulichowaruzuku cha hawa wanyama howa na wamshukuru. Basi Mola wenu, enyi watu, ni Mola Mmoja, Yeye ni Allah Mtukufu. Hivyo basi ifuateni amri Yake na amri ya Mtume Wake. Na uwape bishara njema, ewe Mtume, wale wanyenyekevu waliosalimu amri kwa Mola wao, kwamba watapata kheri mbili: ya ulimwenguni na ya Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net