Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 33

Al-Hajj 22:33

الحج

لَكُمْ فِيهَا مَنَـٰفِعُ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى ثُمَّ مَحِلُّهَآ إِلَى ٱلْبَيْتِ ٱلْعَتِيقِ

Maana

Katika hao nyinyi mna manufaa mpaka muda maalumu. Kisha mahali pa kuchinjiwa kwake ni kwenye Nyumba ya Kale.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Katika hao nyinyi mna manufaa mpaka muda maalumu. Kisha pahala pa kuchinjiwa kwake ni kwenye Nyumba ya Kale. [33]

[33] Katika kutoa mihanga hii yapo manufaa ya kidunia. Mnawapanda na mnakunywa maziwa yake mpaka wakati wa kuwachinja. Kisha mnapata manufaa ya Kidini vile vile pale mnapo wachinja kwenye Nyumba Takatifu kwa kutafuta kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Muna nyinyi, katika wanyama hawa wa kutolewa tunu, manufaa ya nyinyi kunufaika nayo miongoni mwa sufi, maziwa, kipando na mengineyo ambayo hayawadhuru hao wanyama mpaka wakati wa kuchinjwa huko kwenye Nyumba ya kale, nako ni eneo lote takatifu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net