Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 32

Al-Hajj 22:32

الحج

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَـٰٓئِرَ ٱللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى ٱلْقُلُوبِ

Maana

Ndiyo hivyo! Na anayetukuza alama za dini za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo. [32]

[32] Hakika mwenye kuitukuza Dini ya Mwenyezi Mungu na faridha ya Hija na a'mali zake na mihanga inayo pelekwa kwa ajili mafakiri wa Al-Haram, na wakachagua walio nona wazima, hawana ila, basi huyo ndio amemcha Mwenyezi Mungu. Kwani kutukuza kwake hayo ni matokeo ya unyenyekevu wa nyoyo zilizo amini, na alama katika alama za usafi wa niya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hayo ndiyo Aliyoyaamrisha Allah Mtukufu ya kumpwekesha na kumtakasia ibada. Na yoyote mwenye kutekeleza amri ya Allah Mtukufu na akayatukuza mambo makubwa ya Dini, na miongoni mwayo ni matendo ya Hija na sehemu zake na wanyama wanaochinjwa huko, kwa kuchagua walio wazuri na walio wanono, basi kutukuza huko ni katika vitendo vya wenye nyoyo zenye kusifika kwa kumcha Allah Mtukufu na kumuogopa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net