Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 31

Al-Hajj 22:31

الحج

حُنَفَآءَ لِلَّهِ غَيْرَ مُشْرِكِينَ بِهِۦ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِٱللَّهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَتَخْطَفُهُ ٱلطَّيْرُ أَوْ تَهْوِى بِهِ ٱلرِّيحُ فِى مَكَانٍ سَحِيقٍ

Maana

Kwa kumtakasikia Imani Mwenyezi Mungu, bila ya kumshirikisha. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, basi ni kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, kisha ndege wakamnyakua au upepo ukamtupa mahali mbali mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa kumtakasikia Imani Mwenyezi Mungu, bila ya kumshirikisha. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu ni kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, kisha ndege wakamnyakua au upepo ukamtupa pahala mbali. [31]

[31] Na kuweni wenye kumsafia niya Mwenyezi Mungu, wenye pupa kutaka kuifuata Haki, bila ya kumfuata mshirika wowote na Mwenyezi Mungu katika ibada. Kwani mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu ameanguka huyo kutoka kwenye ngome ya Imani, na amesalitiwa na upotovu, na ameitia nafsi yake katika hilaki ya kutisha kabisa. Ikawa hali yake kama hali ya mtu aliye poromoka kutoka mbinguni na midege ikamrarua akakatika mapande mapande, asibakie hata alama. Au kama aliye peperushwa na upepo mkali, na mwili ukatawanyika mwahala mbali mbali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hali ya kulingana sawa kwao katika kumtakasia Allah matendo, kumuelekea Yeye kwa kumuabudu Peke Yake na kumpwekesha kwa utiifu na kumuepuka kila asiyekuwa Yeye kwa kukataa ushirikina, kwani mwenye kumshirikisha Allah Mtukufu na chochote, mfano wake- katika kuwa mbali kwake na uongofu na katika kuangamia kwake na kuanguka kwake kutoka kwenye kilele cha Imani hadi kwenye shimo la ukafiri na wakawa Mashetani wanamnyakua kutoka kila upande - ni kama mfano wa mtu aliyeanguka kutoka mbinguni, ima ndege watamnyakuwa na kumkatakata viungo vyake, au kimbunga kikali cha upepo kitamchukua kimtupe mahali mbali sana.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net