Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 30

Al-Hajj 22:30

الحج

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَـٰتِ ٱللَّهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُۥ عِندَ رَبِّهِۦ ۗ وَأُحِلَّتْ لَكُمُ ٱلْأَنْعَـٰمُ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ ۖ فَٱجْتَنِبُوا۟ ٱلرِّجْسَ مِنَ ٱلْأَوْثَـٰنِ وَٱجْتَنِبُوا۟ قَوْلَ ٱلزُّورِ

Maana

Ni hivyo! Na anayevitukuza vitakatifu vya Mwenyezi Mungu, basi hayo ndiyo heri yake mbele ya Mola wake Mlezi. Na mmehalalishiwa wanyama wa mifugo ila wale mliosomewa. Basi jiepusheni na uchafu wa masanamu, na jiepusheni na usemi wa uongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ndio hivyo iwe! Na anaye vitukuza vitakatifu vya Mwenyezi Mungu basi hayo ndiyo kheri yake mbele ya Mola wake Mlezi. Na mmehalalishiwa nyama hoa ila wale mlio somewa. Basi jiepusheni na uchafu wa masanamu, na jiepusheni na usemi wa uwongo. [30]

[30] Na mwenye kuzishika amri za Mwenyezi Mungu na makatazo yake katika Hija yake kwa kuzitukuza katika nafsi yake, hayo yatakuwa ni kheri yake katika dunia yake na Akhera yake. Na Mwenyezi Mungu amekuhalalishieni kula nyama hoa, (mifugo) yaani ngamia, ng'ombe, kondoo na mbuzi, ila katika hali mnazo zijua kwa mlivyo kwisha somewa katika Qur'ani, kama vile nyamafu na nyenginezo. Basi epukaneni na kuabudu masanamu, kwani ibada hiyo ni uchafu wa kiakili na kiroho, na haimwelekei mwanaadamu kufanya hivyo. Na epukaneni na kusema uwongo, kumzulia Mwenyezi Mungu au mwanaadamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hayo aliyoyaamrisha Allah Mtukufu ya kuondoa uchafu, kutekeleza nadhiri na kuitufu Nyumba ndiyo Aliyoyapasisha Allah Mtukufu, basi yatukuzeni. Na yoyote mwenye kuyatukuza Aliyoyatakasa Allah Mtukufu, (na miongoni mwayo ni matendo Aliyoyawekea ibada ya Hija kwa kuyatekeleza kikamilifu kwa kumtakasia Allah Mtukufu), basi hilo ni bora zaidi kwake, ulimwenguni na Akhera. Na Allah Mtukufu Amewahalalishia nyinyi kula wanyama howa isipokuwa kile Alichokiharamisha kwenu katika kile mnachosomewa ndani ya Qur’ani, miongoni mwa mizoga na mengineyo, basi kiepukeni. Katika hili pana kubatilisha kile ambacho Waarabu walikuwa wakikiharamisha cha baadhi ya wanyama howa. Na jiwekeni mbali na uchafu ambao ni masanamu, na urongo wa kumzulia Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net