Al-Hajj 22:29
الحجثُمَّ لْيَقْضُوا۟ تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا۟ نُذُورَهُمْ وَلْيَطَّوَّفُوا۟ بِٱلْبَيْتِ ٱلْعَتِيقِ
Kisha wajisafishe taka zao, na watimize nadhiri zao, na waizunguke Nyumba ya Kale.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha wajisafishe taka zao, na waondoe nadhiri zao, na waizunguke Nyumba ya Kale. [29]
[29] Tena baada ya hao yawapasa waondoe takataka na uchafu ulio wapata wakati ule wa Ih'ram (yaani kuharimia Hija), nao ni majasho na safari ndefu. Pia waondoe nadhiri walizo mwekea Mwenyezi Mungu, ikiwa wameweka nadhiri yoyote. Na waizunguke kwa kwenda kwa miguu ile Nyumba iliyo jengwa kwa ajili ya ibada ya Mwenyezi Mungu duniani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha wale mahujaji wakamilishe matendo ya ibada yaliyosalia ya kujifungua na kutoka kwenye kifungo cha ibada yao ya Hija, nako ni kwa kuondoa uchafu uliokusanyika kwenye miili yao, kukata kucha zao na kunyoa nywele zao, na watekeleze yale waliyojilazimsha nafsi zao ya kuhiji na kufanya Umra na kuchinja wanyama wa tunu, na waitufu kwa kuizunguka Nyumba huru ya kale ambayo Allah Mtukufu Ameikomboa isitawaliwe kimabavu na watu wasioijali, nayo ni Alkaba.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net