Al-Hajj 22:28
الحجلِّيَشْهَدُوا۟ مَنَـٰفِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا۟ ٱسْمَ ٱللَّهِ فِىٓ أَيَّامٍ مَّعْلُومَـٰتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّنۢ بَهِيمَةِ ٱلْأَنْعَـٰمِ ۖ فَكُلُوا۟ مِنْهَا وَأَطْعِمُوا۟ ٱلْبَآئِسَ ٱلْفَقِيرَ
Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya wanyama wa mifugo aliowaruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama hoa alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri. [28]
[28] Ili wapate manufaa yao ya Kidini kwa kutekeleza Hija na manufaa ya kiduniani kwa kujuana na ndugu zao Waislamu na kushauriana nao katika mambo ya Dini yao na dunia yao. Nao wataje jina la Mwenyezi Mungu katika Siku ya Idi Kubwa na siku tatu zifwatazo, pale wanapo chinja walio jaaliwa, ikiwa ngamia, au ng'ombe au kondoo na mbuzi. Kuleni mpendacho katika hao, na muwalishe walio patwa na shida na ufakiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ili kuyahudhuria yenye kuwafaa ya kusamehewa dhambi zao, kulipwa thawabu za utekelezaji wa ibada yao ya Hija na utiifu wao, kujipatia mapato katika biashara zao na mengine yasiokuwa hayo. Na ili wataje jina la Allah Mtukufu kwa kuchinja wanyama ambao kwao wanajisogeza karibu na Allah Mtukufu, miongoni mwa ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo, katika siku maalumu: nazo ni siku ya kumi ya Mfungotatu na siku tatu baada yake, kwa kumshukuru Allah Mtukufu kwa neema Zake. Na wao wameamrishwa kwa kupendekezewa kula katika vichinjwa hivi, na kumlisha kutokana nazo masikini ambaye umasikini wake umembana.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net