Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 27

Al-Hajj 22:27

الحج

وَأَذِّن فِى ٱلنَّاسِ بِٱلْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِن كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ

Maana

Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliye konda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali. [27]

[27] Ewe Nabii! Wajuvye watu kwamba hakika Mwenyezi Mungu amewalazimisha wawezao miongoni mwao waijie hii Nyumba. Basi waitikie wito wako, watakujia kwa miguu na kwa kupanda ngamia aliye konda kwa ajili ya safari ya kutoka mbali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na uwajulishe watu, ewe Ibrãhîm, uwajibu wa Hija juu yao, watakujia kwa kila namna zao, wakiwa wanatembea kwa miguu na wakiwa wanapanda, miongoni mwa ngamia aliyemwepesi kutembea na kufanya kazi na si dhaifu Watakuja kutoka njia ya mbali.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net