Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 26

Al-Hajj 22:26

الحج

وَإِذْ بَوَّأْنَا لِإِبْرَٰهِيمَ مَكَانَ ٱلْبَيْتِ أَن لَّا تُشْرِكْ بِى شَيْـًٔا وَطَهِّرْ بَيْتِىَ لِلطَّآئِفِينَ وَٱلْقَآئِمِينَ وَٱلرُّكَّعِ ٱلسُّجُودِ

Maana

Na pale tulipomweka Ibrahim pahala penye ile Nyumba tukamwambia: Usinishirikishe na chochote; na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu, na wanaokaa hapo kwa ibada, na wanaorukuu, na wanaosujudu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pale tulipomweka Ibrahim pahala penye ile Nyumba tukamwambia: Usinishirikishe na chochote; na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu, na wanao kaa hapo kwa ibada, na wanao rukuu, na wanao sujudu. [26]

[26] Ewe Nabii! Watajie hawa washirikina wanao dai kuwa ati wanamfuata Ibrahim a.s. na wakaifanya Nyumba Takatifu kuwa ni pahala pa kuwekea masanamu yao; watajie kisa cha Ibrahim na Nyumba Takatifu tulipo mwongoza mpaka pahala pake, na tukamuamrisha aijenge, na tukamwambia: Usinishirikishe Mimi na kitu chochote katika ibada. Na isafishe Nyumba yangu na masanamu na uchafu, ili iwe ni pahala pa makusudi ya mwenye kuizunguka kwa kut'ufu, na mwenye kukaa hapo na akafanya ibada.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbuka, ewe Nabii, pindi tulipomuelezea Ibrãhîm, amani imshukie, mahali pa Nyumba, tukamtayarishia yeye mahali hapo, na palikua hapajulikani. Na tulimuamrisha aijenge juu ya misingi ya kumcha Allah Mtukufu na kumpwekesha na aisafishe na ukafiri na mambo ya uzushi na uchafu, ili iwe ni mahali pakunjufu kwa wenye kuizunguka kwa kutufu na wenye kuswali hapo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net