Al-Hajj 22:36
الحجوَٱلْبُدْنَ جَعَلْنَـٰهَا لَكُم مِّن شَعَـٰٓئِرِ ٱللَّهِ لَكُمْ فِيهَا خَيْرٌ ۖ فَٱذْكُرُوا۟ ٱسْمَ ٱللَّهِ عَلَيْهَا صَوَآفَّ ۖ فَإِذَا وَجَبَتْ جُنُوبُهَا فَكُلُوا۟ مِنْهَا وَأَطْعِمُوا۟ ٱلْقَانِعَ وَٱلْمُعْتَرَّ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرْنَـٰهَا لَكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Na ngamia (na ng'ombe) wa zawadi ya Nyumba Tukufu, tumewafanyia kuwa ni kudhihirisha alama za dini ya Mwenyezi Mungu. Kwa hao mna heri nyingi. Basi litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao wanaposimama kwa safu. Na waangukapo kwenye ubavu, kuleni katika hao na walisheni waliokinai na wanaolazimika kuomba. Ndiyo kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa ni kudhihirisha matukuzo kwa Mwenyezi Mungu; kwa hao mna kheri nyingi. Basi litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao wanapo simama kwa safu. Na waangukapo ubavu kuleni katika hao na walisheni walio kinai na wanao lazimika kuomba. Ndio kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru. [36]
[36] Nasi tumefanya uchinjaji ngamia na ng'ombe n.k. katika Hija kuwa ni katika matukuzo ya Dini yalio dhaahiri. Na nyinyi kwa hayo mnajileta karibu na watu. Nanyi katika hao mnapata kheri nyingi katika dunia kwa kuwapanda, na kunywa maziwa yake. Na Akhera mnapata malipo na thawabu kwa kuwachinja na kuwalisha mafakiri. Basi tajeni jina la Mwenyezi Mungu wakati mnapo wapanga kwa safu kwa ajili ya kuwachinja. Mkisha wachinja kuleni sehemu mkitaka, na walisheni mafakiri walio kinai hawaombi, na ambao wanalazimika kuomba kwa haja. Na kama tulivyo fanya kila kitu kiwe kit'iifu kwa tuyatakayo kwa ajili ya manufaa yenu, na tumedhalilisha hivyo vikut'iini nyinyi ili mpate kuishukuru neema yetu kubwa iliyo juu yenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tumewafanyia nyinyi kule kuchinja ngamia ni miongoni mwa alama za Dini na mambo yake makubwa. Ili mpate kujisogeza karibu na Allah Mtukufu kwayo. Katika hilo, enyi wenye kujikurubisha naye, muna kheri katika manufaa yake ya kula, kutoa sadaka na kupata malipo ya thawabu. Basi semeni mnapowachinja, «Bismillâh» (kwa jina la Allah Mtukufu). Na ngamia huchinjwa akiwa amesimama, miguu yake mitatu imepangwa na mmoja umefungwa, basi akianguka kwa mbavu zake, huwa amekuwa halali kumla. Wale waliomchinja kwa ajili ya ibada na wale kitu katika mnyama huyo na wamlishe kutokana naye aliyekinai, naye ni mhitaji asiyeomba kwa kujihifadhi, na mhitaji anayeomba kumaliza haja yake. Hivi ndivyo Alivyowadhalilishia Allah Mtukufu ngamia, huenda mkamshukuru Allah Mtukufu kwa kuwadhalilishia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net