Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 37

Al-Hajj 22:37

الحج

لَن يَنَالَ ٱللَّهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَآؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ ٱلتَّقْوَىٰ مِنكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمْ لِتُكَبِّرُوا۟ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمْ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُحْسِنِينَ

Maana

Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia ucha Mungu wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyowaongoa. Na wabashirie wafanyao mema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia uchamngu wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyo kuongoeni. Na wabashirie wafanyao mema. [37]

[37] Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu haangalii sura zenu wala vitendo vyenu, lakini anaangalia nyoyo zenu. Wala hataki kwenu mambo ya kujionyesha tu kwa kuchinja na kumwaga damu. Lakini anataka kwenu moyo wenye kunyenyekea. Basi hapati radhi yake mwenye kugawa hizo nyama wala damu. Lakini linalo pata radhi yake ni uchamngu wenu na usafi wa niya zenu. Kuwadhalilisha hao wanyama tulivyo wadhalilisha ni kwa ajili ya kukunafiisheni, mpate kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa vile alivyo kuongoeni hata mkatimiza ibada za Hija. Na ewe Nabii! Wape khabari njema watu wema walio tengeneza a'mali zao na niya zao kuwa watapata malipo makuu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hazitamfikia Allah Mtukufu nyama za vichinjwa hivi wala damu zake kitu chochote, kitakachomfikia Yeye ni kule kumtakasia kwenu katika hivyo na kuwa lengo lake ni radhi za Allah Mtukufu Peke Yake. Hivyo basi Amewadhalilishia nyinyi, enyi wenye kujikurubisha, ili mumtukuze Allah Mtukufu na mumshukuru kwa kuwaongoza kwenye haki, kwani Yeye Anastahiki hilo. Na uwape bishara njema, ewe Nabii, wenye kufanya wema kwa kumuabudu Allah Mtukufu Peke Yake na kuwafanyia wema viumbe vyake, kupata kila jema na kufaulu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net