Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 60

Al-Baqara 2:60

البقرة

وَإِذِ ٱسْتَسْقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦ فَقُلْنَا ٱضْرِب بِّعَصَاكَ ٱلْحَجَرَ ۖ فَٱنفَجَرَتْ مِنْهُ ٱثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۖ كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ مِن رِّزْقِ ٱللَّهِ وَلَا تَعْثَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ مُفْسِدِينَ

Maana

Na Musa alipoomba maji kwa ajili ya watu wake, tukamwambia: 'Lipige jiwe kwa fimbo yako.' Mara zikatimbuka chemichemi kumi na mbili; kila kabila likajua mahali pake pa kunywea. Tukawaambia: Kuleni na mnywe katika riziki ya Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Musa alipo omba maji kwa ajili ya watu wake, tulimwambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikatimbuka chemchem kumi na mbili; kila kabila ikajua mahali pake pa kunywea. Tukawaambia: Kuleni na mnywe riziki ya Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu. [60]

[60] Na kumbukeni, enyi Wana wa Israili, siku Nabii wenu Musa alipo taka maji kutokana na Mola wake Mlezi kiliposhtadi kiu jangwani, Nasi tukakurehemuni. Tukamwambia Musa: Lipige jiwe kwa fimbo yako, yakatimbuka maji kutoka chemchem kumi na mbili. Kila kikundi na chemchem yake, na walikuwa makundi thinaashara Kumi na mbili. Basi kila kabila ikawa na pahala pake pa kunywea. Na tukakwambieni: Kuleni Manna na Salwa, na kunyweni maji haya yanayo timbuka, na muwache mlio nayo, wala msipite mipaka kwa uharibifu katika nchi, bali wacheni maasia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbukeni neema Yetu kwenu, mlipokuwa na kiu katika kuzunguka kwenu, alipotuomba Mûsã, kwa unyenyekevu, tuwaletee maji watu wake. Tukasema, “Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako.”Akalipiga, na chemchemi zikabubujika hapo jiweni sehemu kumi na mbili, ikilingana na idadi ya makabila yao, pamoja na kulijulisha kila kabila chemchemi yake ya kutumia, ili wasigombane. Na tukawaambia, “Kuleni na kunyweni riziki ya Allah Mtukufu wala msitembee katika ardhi kuleta uharibifu.”

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net