Al-Baqara 2:59
البقرةفَبَدَّلَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ قَوْلًا غَيْرَ ٱلَّذِى قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ رِجْزًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُوا۟ يَفْسُقُونَ
Lakini waliodhulumu waliibadili kauli isiyokuwa waliyoambiwa. Kwa hivyo tukaiteremsha juu ya wale waliodhulumu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya walivyokuwa wakivuka mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini walio dhulumu waliibadili kauli isiyo kuwa waliyo ambiwa. Kwa hivyo tukaiteremsha juu ya wale walio dhulumu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya walivyo kuwa wamepotoka. [59]
[59] Lakini walio dhulumu walikwenda kinyume na amri za Mola wao Mlezi, wakasema sio walio amrishwa wayaseme, kwa kudhihaki na kuasi. Basi jaza yao ni kuwa Mwenyezi Mungu aliwateremshia juu yao adhabu kuwa ndiyo malipo ya ukosefu wao na kuzivunja amri za Mola wao Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale wajeuri waliyo wapotevu, katika wana wa Isrãîl, walibadilisha neno la Allah Mtukufu na wakaipotoa kauli pamoja na kitendo. Kwani waliingia, na huku wakijikokota kwa makalio na wakisema, “habbah fî sha’rah’ (mbegu unyweleni.)”, wakiifanyia maskhara dini ya Allah Mtukufu. Allah Mtukufu Aliwateremshia adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya kuasi kwao na kutoka kwao kwenye utiifu kwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net