Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَإِذِ ٱسْتَسْقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦ فَقُلْنَا ٱضْرِب بِّعَصَاكَ ٱلْحَجَرَ ۖ فَٱنفَجَرَتْ مِنْهُ ٱثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۖ كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ مِن رِّزْقِ ٱللَّهِ وَلَا تَعْثَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ مُفْسِدِينَ 60
(60) "Istasqaa" yani (Musa) alipoomba maji ili wanywe kwayo "tulimwambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako." Ima jiwe mahususi analolijua, au jiwe lolote lile "Mara zikatimbuka chemichemi kumi na mbili." Na makabila ya Wana wa Israili yalikuwa kumi na mawili. "Kila kabila" miongoni "likajua mahali pake pa kunywea," katika hizo chemichemi. Kwa hivyo, hawasongamani wao kwa wao, bali wanakunywa kwa furaha siyo kwa kukasirikiana. Na ndio kwa maana akasema: "Kuleni na mnywe katika riziki ya Mwenyezi Mungu." Yani ambayo amekupeni bila ya juhudi wala kutaabika "wala msiende katika ardhi," yani mkifanya uharibifu.