Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 42

Al-Baqara 2:42

البقرة

وَلَا تَلْبِسُوا۟ ٱلْحَقَّ بِٱلْبَـٰطِلِ وَتَكْتُمُوا۟ ٱلْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

Maana

Wala msichanganye haki na batili, na mkaificha haki nanyi mnajua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua. [42]

[42] Wala msichanganye Haki iliyo toka kwangu na upotovu mlio uzua nyinyi, hata ikawa halijuulikani la kweli na la uwongo. Wala msiifiche Haki, na katika hiyo Haki ni kumsadiki Muhammad, na nyinyi mnajua kuwa yeye ni wa kweli na wa kusadikiwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala msichanganye haki niliyowafafanulia, na batili mliyoizusha. Na jihadharini kuificha haki iliyo wazi ya sifa za Nabii na Mtume wa Allah Mtukufu, Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ambazo zimo ndani ya vitabu vyenu. Na nyinyi mnazipata hizo zimeandikwa kwenu, katika vitabu mnavyovijua vilivyoko mikononi mwenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net