Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 43

Al-Baqara 2:43

البقرة

وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱرْكَعُوا۟ مَعَ ٱلرَّٰكِعِينَ

Maana

Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na inameni pamoja na wanaoinama.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na shikeni Swala, na toeni Zaka, na inameni pamoja na wanao inama. [43]

[43] Itikieni Imani. Shikeni Swala yenye nguzo zilizo simama baraabara. Na toeni Zaka muwape wanao stahiki. Na salini pamoja na jamaa wa Kiislamu ili mpate malipo ya Swala na thawabu za kusali jamaa. Na haya yanalazimu kuwa muwe Waislamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ingieni kwenye dini ya Uislamu: Msimamishe Swala kwa njia sahihi kama alivyokuja nayo Nabii wa Allah Mtukufu na Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, mtekeleze Zaka za lazima kwa namna iliyowekwa na Sheria, na mue pamoja na wanaorukuu katika ummah wake, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net