Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 43

وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱرْكَعُوا۟ مَعَ ٱلرَّٰكِعِينَ 43

(43) Kisha akasema "Na shikeni Sala," yani kwa nje na kwa ndani "na toeni Zaka" muwape wanaoistahiki "na inameni (rukuuni) pamoja na wanaoinama." Yani swalini pamoja na wanaoswali. Kwa sababu, mkifanya hivyo kwa kuwaamini Mitume wa Mwenyezi Mungu na Ishara (aya) za Mwenyezi Mungu, basi mtakuwa mmekusanya kati ya matendo ya nje na ya ndani (yaliyofichika), na kati ya kumpwekesha muabudiwa (yani Mwenyezi Mungu), na kuwafanyia wema waja wake. Na kati ya ibada za moyoni, kiwiliwili, na kimali. Na kauli yake, "na inameni (rukuuni) pamoja na wanaoinama." Maana yake ni swalini pamoja na wanaoswali. Basi ndani yake imo amri ya kuswali katika Jamaa (mkusanyiko) na ulazima wake. Na ndani yake kuna kwamba rukuu ni katika nguzo za swala; kwa sababu yeye alizungumzia swala kwa kutaja rukuu. Na kuzungumzia ibada kwa kutaja sehemu yake kunaonyesha ulazima wake ndani yake.