Al-Baqara 2:41
البقرةوَءَامِنُوا۟ بِمَآ أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوٓا۟ أَوَّلَ كَافِرٍۭ بِهِۦ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِى ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّـٰىَ فَٱتَّقُونِ
Na aminini niliyoyateremsha ambayo yanasadikisha mliyo nayo, wala msiwe wa kwanza kuyakataa. Wala msiuze ishara zangu kwa thamani ndogo. Na nicheni Mimi tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na aminini niliyo yateremsha ambayo yanasadikisha mliyo nayo, wala msiwe wa kwanza kuyakataa. Wala msiuze Ishara zangu kwa thamani ndogo. Na niogopeni Mimi tu. [41]
[41] Na isadikini Qur'ani iliyo teremshwa kusadikisha vile vitabu mlivyo navyo, na kufunza Tawhidi (kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja) na kumwabudu Mwenyezi Mungu, na uadilifu baina ya watu. Wala msikimbilie kutaka kuipinga Qur'ani msije mkawa ndio wa mwanzo kuikana, na ilhali ifaavyo ni nyinyi ndio muwe wa mwanzo kuiamini. Wala msiziache Ishara za Mwenyezi Mungu mkenda badala yake mkachukua chenginecho kipitacho njia katika starehe za uhai wa dunia. Na niogopeni Mimi tu, na fuateni Njia yangu, na wacheni upotovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na iaminini Qur,ani, enyi wana wa Isrãîl, ambayo niliiteremsha kwa Muhammad, aliye Nabii na Mtume wa Allah Mtukufu, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie yeye, ambayo inalingana na yale mnayoyajua yaliyo sahihi katika Taurati. Na msiwe ni kundi la mwanzo la Watu wa Kitabu (ahl al-kitāb) kuikanusha. Na wala msizibadilishe aya zangu kwa thamani chache ya taka za dunia zenye kuondoka. Na Kwangu Mimi, Peke Yangu, fanyeni vitendo vya kunitii na acheni kuniasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net