Al-Baqara 2:40
البقرةيَـٰبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتِىَ ٱلَّتِىٓ أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا۟ بِعَهْدِىٓ أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّـٰىَ فَٱرْهَبُونِ
Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni neema yangu niliyokuneemesheni, na timizeni agano langu, na Mimi nitatimiza agano lenu, na niogopeni Mimi tu.[1]
[1] “Enyi Wana wa Israili!” Anayekusudiwa na Israili hapa ni Nabii Yaaqub, amani iwe juu yake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni neema yangu niliyo kuneemesheni, na timizeni ahadi yangu, na Mimi nitatimiza ahadi yenu, na niogopeni Mimi tu. [40]
[40] Enyi Wana wa Israili kumbukeni neema zangu nilizo kutunukieni nyinyi na wazee wenu kwa kuzifikiri na kushukuru na kutimiza agano langu nililo lichukua kwenu, na nyinyi nafsi zenu mkalikiri, nalo ni Imani, na Vitendo vyema, na kuwasadiki Manabii wajao baada ya Musa, ili Nami nitimize ahadi yangu kwenu, nayo ni kukulipeni malipo mema, na neema ya kudumu. Na wala msimwogope mtu yeyote isipo kuwa Mimi, na tahadharini na kufanya mambo yatakayo nifanya nikasirike nanyi. Aya hii inaonyesha kuwa ahadi, au agano, ni waajibu wa pande zote mbili zilizo ahidiana kutimiza lilio lazimika. Akiacha mmojapo basi haimlazimu wa pili kutimiza agano lake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi kizazi cha Ya‛qûb, kumbukeni neema za Allah Mtukufu zilizo nyingi kwenu, nishukuruni na timizeni wasia Wangu kwenu kuwa muviamini Vitabu Vyangu na Mitume Wangu Wote, mfuate Sheria Zangu kivitendo. Mkifanya hivyo, nitawatimizia niliyowaahidi ya kuwarehemu katika ulimwengu na kuwaokoa kesho Akhera. Na Mimi, Peke Yangu, niogopeni na muwe na hadhari na mateso Yangu ikiwa mtavunja ahadi na kunikanusha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net