Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 37

Al-Baqara 2:37

البقرة

فَتَلَقَّىٰٓ ءَادَمُ مِن رَّبِّهِۦ كَلِمَـٰتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Maana

Kisha Adam akapokea maneno kutoka kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi akamkubalia toba yake; Hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu. [37]

[37] Adam na mkewe walitambua makosa yao na kujidhulumu nafsi zao. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfunza Adam baadhi ya maneno ya kutubia na kuomba msamaha na akayasema. Mwenyezi Mungu alimkubalia toba yake, na akamsamehe, kwani Yeye ni mwingi wa kukubali toba, naye ni Mwenye kuwarehemu waja wake wanyonge.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ãdam alipokea matamko ya kuomba ili akubaliwe, aliyoletewa na Allah Mtukufu, kwa njia ya ilham (ilhām), yaliyokusanya toba na kutaka msamaha, nayo ni neno Lake Aliyetukuka, “Ewe Mola wetu! Tumejidhulumu nafsi zetu. Na Usipotusamehe na Kuturehemu, hakika tutakuwa ni miongoni mwa waliyopata hasara.” (7:23). Allah Mtukufu Alikubali toba yake na Akamsamehe. Kwani Yeye, Aliyetukuka, ni Mwingi wa kukubali toba ya Mwenye kutubia miongoni mwa waja Wake na ni Mwenye Kuwarehemu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net