Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
فَتَلَقَّىٰٓ ءَادَمُ مِن رَّبِّهِۦ كَلِمَـٰتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ 37
(37) “Kisha Adam akapokea,” yani Mwenyezi Mungu alimfunulia “maneno kutoka kwa Mola wake Mlezi;” nayo ni kauli yake: “Mola wetu Mlezi, Tumezidhulumu nafsi zetu” hadi mwisho wa aya. Kwa hivyo, akakiri dhambi zake, na akamuomba Mwenyezi Mungu msamaha juu yake. “Na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake” na akamrehemu “hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba;” kwa mwenye kutubia kwake na akarejea kwake. Na toba yake ni ya aina mbili: Kumwezesha kwanza, kisha pili kukubali kwake (Mwenyezi Mungu) toba hiyo ikiwa itajumuisha masharti yake. “Na Mwenye kurehemu,” kwa waja wake. Na katika rehema yake juu yao ni kuwawezesha kutubu, na akawasamehe, na akaachilia.