Al-Baqara 2:36
البقرةفَأَزَلَّهُمَا ٱلشَّيْطَـٰنُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ ۖ وَقُلْنَا ٱهْبِطُوا۟ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَـٰعٌ إِلَىٰ حِينٍ
Lakini Shetani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyokuwamo, na tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika ardhi yatakuwa makazi yenu na starehe kwa muda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini Shet'ani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyo kuwamo, na tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu na starehe kwa muda. [36]
[36] Lakini Iblis, anaye mhusudu na kumchukia Adam, alimfanyia vitimbi, akawadanganya mpaka wakateleza wakala mti walio katazwa. Mwenyezi Mungu akawatoa katika ile neema na ukarimu walio kuwa nayo. Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaamrisha washukie kwenye Ardhi waishi humo wao na vizazi vyao, na wawe na uadui baina yao kwa wao kwa sababu ya ushindani na kupotozwa na Shetani. Na huko kwenye Ardhi pawe pahali pa kukaa kwao na kupata maisha, na kustarehe kutako kwisha kwa kutimia wakati.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Shetani akawaingiza makosani, kwa kuwashawishi mpaka wakala katika ule mti, ikasababisha kutolewa kwao kwenye Pepo na starehe zake. Na Allah Mtukufu Aliwaambia, “Shukeni ardhini, mkiteta nyinyi kwa nyinyi- yaani: Adam, Ḥawwā’ na Shetani-, na nyinyi katika hiyo ardhi muna utulivu na makao na kunufaika kwa vilivyomo mpaka muda wa maisha yenu ukome.”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net