Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 35

Al-Baqara 2:35

البقرة

وَقُلْنَا يَـٰٓـَٔادَمُ ٱسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ ٱلْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale waliodhulumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio dhulumu. [35]

[35] Kisha Mwenyezi Mungu alimuumba Adam na mkewe, na akawaamrisha wakae katika Bustani ya neema. Akamwambia: Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii na kuleni humo mtakavyo vya kutosha bila ya kutaabika, na kaeni mtakapo, mle mtakacho. Lakini Mwenyezi Mungu aliwatajia mti maalumu na akawahadharisha wasiule, na akawaambia: Msiukaribie mti huu, wala msile matunda yake. Mkifanya hivyo mtakuwa miongoni mwa walio dhulumu, na mtakuwa waasi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Akasema, “Ewe Ãdam! Kaa wewe na mkeo Ḥawwā’ kwenye pepo na stareheni kwa matunda yake kwa furaha na ukunjufu popote pale mnapotaka humo, na tahadharini na mti huu, msije mkaingia katika maasia mkawa ni wenye kukiuka amri ya Allah Mtukufu.”

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net