Al-Baqara 2:34
البقرةوَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسْجُدُوا۟ لِـَٔادَمَ فَسَجَدُوٓا۟ إِلَّآ إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَٱسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلْكَـٰفِرِينَ
Na tulipowaambia Malaika: 'Msujudieni Adam', wakamsujudia wote isipokuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri. [34]
[34] Na kumbuka Ewe Nabii! Tulipo waambia Malaika: Mnyenyekeeni Adamu kwa kumwamkia na kuukiri ubora wake. Wakat'ii Malaika wote ila Iblis. Yeye alikataa kusujudu akawa miongoni mwa walio asi, walio zikataa neema za Mwenyezi Mungu, na hikima yake, na ujuzi wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, takrima ya Allah Mtukufu kwa Ãdam Aliposema Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kuwaambia Malaika, “Msujudieni Ãdam kwa njia ya kumheshimu na kuonyesha fadhila zake.” Wote walitii amri, isipokuwa Iblisi alikataa kusujudu kwa sababu ya kiburi na uhasidi, akawa ni miongoni mwa wenye kumkanusha Allah Mtukufu, wenye kuasi amri Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net