Al-Baqara 2:33
البقرةقَالَ يَـٰٓـَٔادَمُ أَنۢبِئْهُم بِأَسْمَآئِهِمْ ۖ فَلَمَّآ أَنۢبَأَهُم بِأَسْمَآئِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّىٓ أَعْلَمُ غَيْبَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ
Akasema: 'Ewe Adam! Waambie majina yake.' Basi alipowaambia majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani, na ninayajua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mnayaficha?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Ewe Adam! Waambie majina yake. Basi alipo waambia majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani, na ninayajua mnayo yadhihirisha na mliyo kuwa mnayaficha? [33]
[33] Mwenyezi Mungu alimwambia Adam: Watajie Malaika khabari za vitu hivi. Akataja; na ukadhihiri ubora wake juu yao. Na hapo Mwenyezi Mungu akawaambia kuwakumbusha vipi ujuzi wake ulivyo enea: Sikukwambieni kuwa Mimi ninajua siri za mbingu na ardhi, na hapana ajuae hayo isipo kuwa Mimi, na Mimi ninajua mnayo yadhihirisha katika kauli yenu, na mnayo yaficha katika nafsi zenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Alisema, “Ewe Ãdam! Waambie majina ya vitu hivi ambayo walishindwa kuyajua.” Ãdam alipowaambia hayo majina, Allah Mtukufu Alisema kuwaambia Malaika, “Niliwaambia kuwa Mimi ninayajua yaliyofichika kwenu, ya mbinguni na ardhini, na ninayajua mnayoyafanya kwa dhahiri na mnayoyafanya kwa siri.”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net