Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 33

قَالَ يَـٰٓـَٔادَمُ أَنۢبِئْهُم بِأَسْمَآئِهِمْ ۖ فَلَمَّآ أَنۢبَأَهُم بِأَسْمَآئِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّىٓ أَعْلَمُ غَيْبَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ 33

(33) Na hapo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema “Ewe Adam! Waambie majina yavyo.” Yani majina ya vile vilivyotajwa, ambavyo Mwenyezi Mungu aliviweka mbele ya Malaika; nao wakashindwa kuvitaja majina. “Basi alipowaambia majina yake,” ukawabainikia Malaika ubora wa Adam juu yao, na hekima na elimu ya Al-Bari (Muumbaji) katika kumteua huyu khalifa. “Alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani.” Nayo (ghaibu) ni kila kilichofichikana kwetu; tukawa hatukioni. Na ikiwa (Yeye Mwenyezi Mungu) anajua ghaibu; basi ya dhahiri yanastahiki zaidi (yeye kuyajua). “Na ninayajua mnayoyadhihirisha,” yani mnayoweka wazi; “na mliyokuwa mnayaficha.”