Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 38

Al-Baqara 2:38

البقرة

قُلْنَا ٱهْبِطُوا۟ مِنْهَا جَمِيعًا ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّى هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَاىَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

Maana

Tukasema: Shukeni nyote kutoka humo; na kama ukikufikieni uongofu utokao kwangu, basi watakaofuata uongofu wangu huo, haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. [38]

[38] Tukamwambia Adam na mkewe na vizazi vyao vijavyo na Iblis: Shukeni katika Ardhi, na huko mtalazimishwa mambo. Yakikujieni hayo kutokana na Mimi - na hapana shaka yatakujieni - basi wale watakao itikia amri yangu, na wakafuata uwongofu wangu hawataona khofu yoyote, na hawatopata huzuni, kwa kukosa thawabu, kwa sababu Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa atendaye mema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tulisema, “Shukeni kutoka Peponi nyote! Na utawajia, nyinyi na vizazi vyenu vinavyofuatia, ujumbe wenye mambo ya kuwaongoza kwenye haki. Wenye kuufuata huo kwa vitendo, hawatakuwa na hofu kuhusu mustakbala wao wa Akhera, wala hawatakuwa na huzuni juu ya vitu walivyovikosa vya ulimwenguni.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net