Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 273

Al-Baqara 2:273

البقرة

لِلْفُقَرَآءِ ٱلَّذِينَ أُحْصِرُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِى ٱلْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ ٱلْجَاهِلُ أَغْنِيَآءَ مِنَ ٱلتَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَـٰهُمْ لَا يَسْـَٔلُونَ ٱلنَّاسَ إِلْحَافًا ۗ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٌ

Maana

Na wapewe mafakiri waliozuiliwa katika njia za Mwenyezi Mungu, wasioweza kusafiri katika nchi kutafuta riziki. Asiyewajua hali zao huwadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao. Utawatambua kwa alama zao; hawawang'ang'anilii watu kwa kuwaomba. Na chochote mnachotoa katika heri, basi hakika Mwenyezi Mungu anaijua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nawapewe mafakiri walio zuilika katika njia za Mwenyezi Mungu, wasio weza kusafiri katika nchi kutafuta riziki. Asiye wajua hali zao huwadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao. Utawatambua kwa alama zao; hawang'ang'analii watu kwa kuwaomba. Na kheri yoyote mnayo toa, basi kwa yakini Mwenyezi Mungu anaijua. [273]

[273] Na kutoa huko ni kwa kuwapa mafakiri ambao kwa sababu ya kuwania jihadi hawawezi kujichumia wenyewe, au ambao kwa sababu ya kuumia katika jihadi wameemewa na kuweza kuhangaika katika nchi kutafuta riziki. Na juu ya hivyo wanajizuia na kuomba omba. Asiye wajua huwadhania kuwa ni matajiri, lakini wewe utajua hali yao kwa alama zake. Na kila mtacho kitoa kwa wema, basi Mwenyezi Mungu anakijua, naye atakulipeni malipo ya kutosha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wapeni sadaka zenu mafukara Waislamu ambao hawawezi kusafiri kutafuta riziki, kwa kuwa wameshughulika na jihadi katika njia ya Allah Mtukufu, ambao huwadhania wao wasiowajua kuwa hawahitaji sadaka kwa kuwa wamejizuia na kuomba.Utawajua kwa alama zao na athari ya uhitaji walionao. Hawaombi kabisa. Na wakiomba, kwa kukosa budi, hawaombi kwa utiriri. Na mali yoyote mnayoyatoa katika njia ya Allah Mtukufu, hakuna chochote, katika hayo, chenye kufichika kwa Allah Mtukufu.Na Allah Mtukufu Atalipa kwayo malipo mengi zaidi na makamilifu zaidi Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net