Al-Baqara 2:274
البقرةٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُم بِٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ سِرًّا وَعَلَانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ
Wale wanaotoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao, wala wao hawatahuzunika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale wanao toa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhaahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. [274]
[274] Wale ambao dasturi yao ni kutoa kwa ukarimu wa nafsi zao usiku na mchana, mbele za watu na katika siri, watapata malipo yao kutokana na Mola wao Mlezi. Hawatofikiwa na khofu yoyote baadae, wala hawatakuwa na huzuni kwa kukosa chochote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale ambao wanatoa mali zao kwa kumridhisha Allah Mtukufu, mchana na usiku, kwa siri na kwa dhahiri, watapata malipo yao mbele ya Mola wao, na wala hapana khofu juu yao kuhusu mambo watakayoyakabili Akhera wala hawatakuwa na huzuni juu ya vitu vya kidunia vilivyowapita wasivipate. Sheria hiyo ya Ki Mungu yenye hekima, ndiyo njia ya Uislamu katika utoaji, yenye kuondoa mahitaji ya mafukara kwa heshima na utu, kusafisha mali ya matajiri na kuhakikisha kusaidiana juu ya wema na ucha Mungu ili kutaka radhi za Allah Mtukufu bila maonevu au kulazimisha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net