Al-Baqara 2:272
البقرةلَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَىٰهُمْ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهْدِى مَن يَشَآءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ ٱللَّهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ
Si juu yako wewe kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na chochote mnachotoa katika heri, basi ni cha nafsi zenu. Wala hamtoi isipokuwa kwa kutafuta uso wa Mwenyezi Mungu. Na chochote mnachotoa katika heri, mtalipwa kwa ukamilifu, nanyi hamtadhulumiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Si juu yako wewe kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na kheri yoyote mnayo toa ni kwa nafsi zenu. Wala msitoe ila kwa kutafuta wajihi wa Mwenyezi Mungu. Na kheri yoyote mtakayo toa mtalipwa kwa ukamilifu, wala hamtadhulumiwa. [272]
[272] Si juu yako wewe, ewe Muhammad, kuwaongoa hao walio potea au kuwalazimisha watende kheri. Lilio juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na msaada wowote mnao toa kumpa mtu, faida yake inarejea kwenu wenyewe. Mwenyezi Mungu atakulipeni kwayo. Haya ni hivyo ikiwa mnapo toa hamkusudii ila kumridhi Mwenyezi Mungu. Na kheri yoyote mnayo itoa kwa njia hii itarejea kwenu, na mtazipata thawabu zake kwa ukamilifu bila ya kudhulumiwa chochote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Si jukumu lako, ewe Mtume, kuwapa makafiri taufiki ya uongofu, lakini Allah Mtukufu Anavifungua vifua vya Anaowataka kwa Dini Yake na kuwaafikia kuifuata. Na mali yoyote mnayoyatoa, nafuu yake itawarudia nyinyi wenyewe kutoka kwa Allah Mtukufu. Na Waumini hawatoi isipokuwa kwa kutafuta radhi ya Allah Mtukufu. Na mali yoyote mnayoyatoa, kwa kumtakasia Allah Mtukufu, mtapewa kikamilifu thawabu zake na hamtapunguziwa chochote katika hizo. Katika hii aya pana kuthibitisha sifa ya Uso kwa Allah Mtukufu Aliyetakasika na kila sifa pungufu (wajh Allãh) kwa namna inayonasibiana na Yeye.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net