Al-Baqara 2:271
البقرةإِن تُبْدُوا۟ ٱلصَّدَقَـٰتِ فَنِعِمَّا هِىَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا ٱلْفُقَرَآءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّـَٔاتِكُمْ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ
Mkizidhihirisha sadaka, basi hilo ni vizuri. Na mkizificha na mkawapa mafakiri kwa siri, basi hilo ni heri kwenu, na yatawaondolea katika maovu yenu. Na Mwenyezi Mungu ana habari ya mnayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri; na mkizificha mkawapa mafakiri kwa siri basi hivyo ni kheri kwenu, na yatakuondoleeni baadhi ya maovu yenu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. [271]
[271] Na ikiwa mtazidhihirisha sadaka zenu, bila ya makusudio ya kutaka kujionyesha kwa watu, ni vizuri kwenu, inapendeza, na kwa Mola wenu Mlezi inasifika. Na pindi mkiwapa mafakiri kwa siri ili msiwatie haya, na kwa kuogopa riya (kujionyesha), basi nayo ni kheri kwenu. Na Mwenyezi Mungu atakusameheni dhambi zenu kwa sababu ya usafi wa niya zenu katika kutoa sadaka zenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yaficha na mnayo yadhihirisha, na anazijua niya zenu mnapo dhihirisha na mnapo ficha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mkizidhihirisha zile mnazozitoa sadaka kwa ajili ya Allah Mtukufu, ni sadaka nzuri mliyoitoa. Na mkizitoa kwa siri mkawapa mafukara, ni bora zaidi kwenu kwa kuwa hivyo ni mbali na ria. Na katika utoaji sadaka pamoja na ikhlasi kuna kusamehewa madhambi yenu. Na Allah Mtukufu Anayajua mambo ya ndani; hakuna kinachofichika Kwake katika mambo yenu na Atamlipa kila mtu kwa amali yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net