Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 270

Al-Baqara 2:270

البقرة

وَمَآ أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُهُۥ ۗ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

Maana

Na chochote mnachotoa au nadhiri mnazoweka, basi hakika Mwenyezi Mungu anajua hayo. Na madhalimu hawana wowote wa kuwanusuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na chochote mnacho toa au nadhiri mnazo weka basi hakika Mwenyezi Mungu anajua. Na walio dhulumu hawana wa kuwanusuru. [270]

[270] Na kila mnacho kitoa, ikiwa kwa kheri au shari, au mnacho lazimika kutoa kwa ut'iifu, basi Mwenyezi Mungu anakijua na atakulipeni. Na wale wenye kudhulumu, wanao toa kwa ajili ya kujionyesha kwa watu au wale wanapo toa wanawaudhi masikini za Mungu, au wanao toa kwa ajili ya maasi, hawatakuwa na watu wa kuwanusuru na adhabu ya Mwenyezi Mungu huko Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mali yoyote mnayoyatoa na mengineyo, machache au mengi, au sadaka mnayoitoa kwa kutaka radhi ya Allah Mtukufu, au mkajilazimisha nafsi zenu chochote, cha mali au kinginecho, basi Allah Mtukufu Anayajua hayo; na Yeye Ndiye Mwenye kujua nia zenu, na Atawalipa kwa hayo.Na yoyote mwenye kuzuia haki ya Allah Mtukufu ni dhalimu. Na madhalimu hawana wenye kuwanusuru ambao watawazuia wasipate adhabu ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net