Al-Baqara 2:269
البقرةيُؤْتِى ٱلْحِكْمَةَ مَن يَشَآءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ ٱلْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِىَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّآ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَـٰبِ
Yeye humpa hekima amtakaye. Na mwenye kupewa hekima, basi bila ya shaka amepewa heri nyingi. Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili ya hali ya juu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye humpa hikima amtakaye; na aliye pewa hikima bila ya shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili. [269]
[269] Yeye humpa sifa ya Hikima, kusema na kutenda lilio la haki, ampendaye kati ya waja wake. Na mwenye kupewa hayo basi kapewa kheri nyingi, kwani kwayo ndio hutengenea mambo ya duniani na Akhera. Na wala hawanafiiki kwa waadhi na mazingatio ya amali za Qur'ani ila wale wenye akili sawa inayo tambua ukweli bila ya kupindukia mipaka kwa pumbao la ufisadi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Anampa taufiki ya usawa katika kunena na kutenda Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na yoyote ambaye Allah Mtukufu Amemneemesha kwa hilo, Hua Amempa kheri nyingi. Na hatakumbuka hilo na kunufaika nalo isipokuwa wenye akili zenye kung’ara kwa nuru ya Allah Mtukufu na uongofu Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net