Al-Baqara 2:268
البقرةٱلشَّيْطَـٰنُ يَعِدُكُمُ ٱلْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِٱلْفَحْشَآءِ ۖ وَٱللَّهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ
Shetani anawatia hofu ya ufakiri, na anawaamrisha machafu. Na Mwenyezi Mungu anawaahidi msamaha kutoka kwake na fadhila. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Shet'ani anakutieni khofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha na fadhila zitokazo kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua. [268]
[268] Shetani anakutieni khofu kuwa mtafakirika kwa kutoa, na kazi yake kutia ila kila kitendo chema, ili msitoe kwa ajili ya mambo ya kheri na mghurike na maasi. Na Mwenyezi Mungu aliye Mkunjufu wa kusamehe, ni Muweza wa kukutoshelezeni. Hapana lolote katika mambo yenu linalo fichikana kwake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Uchoyo huu na kuchagua kibaya kukitoa sadaka yatokana na Shetani ambaye anawaogopesha nyinyi ufukara na kuwahimiza uchoyo, na anawaamrisha nyiyi maasia na kumfanyia kinyume Allah Mtukufu. Na Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Anawaahidi nyinyi, kwa kutoa kwenu, msamaha wa madhambi yenu na riziki kunjufu. Na Allah Mtukufu ni Mwenye nyongeza zenye kuenea, ni Mjuzi wa nia na vitendo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net