Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 267

Al-Baqara 2:267

البقرة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنفِقُوا۟ مِن طَيِّبَـٰتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّآ أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا۟ ٱلْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِـَٔاخِذِيهِ إِلَّآ أَن تُغْمِضُوا۟ فِيهِ ۚ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ حَمِيدٌ

Maana

Enyi mlioamini! Toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyowatolea katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, ilhali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa. [267]

[267] Enyi Waumini! Toeni bora ya mnacho kipata kwa juhudi yenu, na ambacho mlicho wezesha kukitoa katika ardhi, ikiwa kwa makulima, au maadini au chenginecho. Wala msikusudie kutoa kile kilicho duni na kibaya katika mali, na ilhali nyinyi msinge kubali kuchukua hivyo ila ingeli kuwa mmegubikwa macho au hamuuoni huo ubaya. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu si mwenye haja ya sadaka zenu, na Yeye ni mwenye kustahiki kila sifa njema na shukrani kwa alivyo kuongozeni kuendea kheri na wema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlioniamini na mkawafuata Mitume wangu, toeni miongoni mwa halali mliyoichuma na ile tuliyowatolea kutoka kwenye ardhi. Na wala msikusudie kutoa kibaya, katika hiyo halali, kuwapa mafukara, ambacho lau nyinyi mngalipewa, hamngalikipokea isipokuwa mkiwa mtapuuza ubaya na upungufu ulionacho. Ni vipi nyinyi mnaridhika kumpa Allah Mtukufu kitu ambacho hamridhiki nacho mkipewa? Na jueni kwamba Allah Mtukufu Aliyewaruzuku Anajitosha kutohitajia sadaka zenu, ni Mstahiki wa kusifiwa na Mhimidiwa kwa kila hali.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net