Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنفِقُوا۟ مِن طَيِّبَـٰتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّآ أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا۟ ٱلْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِـَٔاخِذِيهِ إِلَّآ أَن تُغْمِضُوا۟ فِيهِ ۚ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ حَمِيدٌ 267 ٱلشَّيْطَـٰنُ يَعِدُكُمُ ٱلْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِٱلْفَحْشَآءِ ۖ وَٱللَّهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ 268
{267 - 268} Al-Bari (Muumba mwanzilishi) anawahimiza waja wake watoe katika yale waliyoyachuma katika biashara, na katika yale aliyowatolea katika ardhi kama vile nafaka na matunda. Na hili linajumuisha Zaka ya dhahabu na fedha na vitu vilivyotayarishwa kwa ajili ya kuuza na kununua, na kinachotoka katika ardhi kama vile nafaka na matunda. Na linajumlisha katika ujumla wake (kutoa kwa) faradhi na sunna. Na Mola Mtukufu aliamrisha kwamba wayakusudie vilivyo vizuri vyake, wala wasikusudie vilivyo vibaya na vilivyo duni; ati ndivyo wanavyompa Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa wao wangepewa hivyo na wale ambao wao wana haki juu yao, basi hawangeviridhia, na wala hawangevikubali isipokuwa kwa njia ya kupepesa na kufumba macho. Basi, la wajibu ni kutoa cha wastani katika mambo haya. Na ukamilifu ni kutoa cha juu, na kilichokatazwa ni kutoa kibaya. Kwa sababu, hili halitoshelezi wajibu, na wala hazipatikani ndani yake thawabu kamili katika lile linalopendekezwa. "Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa." Yeye havihitaji viumbe vyote, na hakuhitaji kutoa kwa wanaotoa, na hauhitaji utiifu wa watiifu. Yeye aliwaamrisha hayo tu na akawahimiza juu yake kwa manufaa yao na fadhila yake tupu na ukarimu juu yao. Na pamoja na ukamilifu wa kujitegemea kwake na upana wa vipawa vyake, Yeye ndiye Msifiwa katika yale anayowawekea waja wake sheria kama vile hukumu zenye kuwafikisha kwenye nyumba ya amani. Naye ni Msifiwa katika vitendo vyake visivyotoka nje ya fadhila, na uadilifu, na hekima. Naye ni mwenye sifa nzuri zaidi kwa sababu sifa zake zote ni nzuri na kamilifu ambazo waja hawafikii dhati zake, na hawafikii maelezo yake. Na alipowahimiza juu ya kutoa kwenye kuwanufaisha, akawakataza kutotoa kwenye kuwadhuru. Na akawabainishia kuwa wao wako baina ya walinganiaji wawili: Mlinganiaji wa Mwingi wa Rehema anayewalingania kwenye heri; na anawaahidi heri kwa hayo na fadhila na thawabu ya haraka na ya baadaye, na kuwarudishia walichotoa. Na mlinganiaji wa Shetani, ambaye anawahimiza juu ya kutotoa, na anawahofisha kwamba wakitoa, watakuwa mafakiri. Hivyo basi, atakayekuwa mwenye kumuitikia mlinganiaji wa Mwingi wa Rehema, na akatoa katika yale aliyomruzuku Mwenyezi Mungu. Basi na awe na bishara njema ya msamaha wa dhambi na kupata kila anachotafuta. Na yeyote atakayemuitikia mlinganiaji wa Shetani, basi yeye kwa hakika analiita kundi lake ili wawe miongoni mwa wenza wa Moto wenye mwako mkali. Basi mja na achague lolote la mambo mawili haya; lile linalomfaa zaidi. Na alihitimisha Aya hiyo kwa kusema; "ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua." Yani mwenye sifa pana, mwingi wa vipawa, mwenye kujua ni nani anayestahiki kuzidishiwa miongoni mwa watendaji matendo. Na mwenye kujua wanaostahiki, kwa hivyo anamuwezesha kufanya mema, na kuacha maovu.