Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 262

Al-Baqara 2:262

البقرة

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَآ أَنفَقُوا۟ مَنًّا وَلَآ أَذًى ۙ لَّهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

Maana

Wale wanaotoa mali zao kwa Njia ya Mwenyezi Mungu, kisha hawafuatishi kile walichotoa masimbulizi wala udhia, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanao toa mali zao kwa Njia ya Mwenyezi Mungu, kisha hawafuatishii masimbulizi wala udhia kwa walicho toa, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. [262]

[262] Hakika wanao toa mali kwa ajili ya wema unao kubaliwa na sharia bila ya kusimbulia au kutafakhari au kumcheleweshea yule anaye fanyiwa hisani, hao wana malipo bora walio ahidiwa kwa Mola wao Mlezi, wala haiwapati khofu kwa lolote wala huzuni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale ambao wanatoa mali yao katika jihadi na aina mbali mbali za kheri, kisha wasifuatishe, yale waliyoyatoa ya kheri, kwa kumsemanga waliyempa wala kumkera, kwa neno au kitendo, kwa kumhisisha kuwa wamemfadhili, watapata thawabu kubwa mbele ya Mola wao na hawatakuwa na hofu kuhusu mustakbali wao wa Akhera wala hawatahuzunika juu ya kitu chochote kilichowapita wasikipate katika ulimwengu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net