Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَآ أَنفَقُوا۟ مَنًّا وَلَآ أَذًى ۙ لَّهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ 262
{262} Kisha pia alitaja malipo mengine kwa wale wanaotoa mali zao kwa ajili ya matumizi katika njia yake. Kutoa ambako kunatoka huku kumetimiza masharti yake na ambako hakuna vizuizi vyake. Basi hawamfuati aliyepewa kwa masimbulizi juu yake na kuhesabu neema na kumuudhi kwa maneno au vitendo. Basi hao “wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi” kulingana na kile anachojua ndani yao. Na kulingana na kile walichotoa na manufaa yake, na kwa fadhila yake ambayo kutoa kwao hakuipati wala hakuifikii “na wala haitakuwa hofu juu yao wala hao hawatahuzunika”. Kwa hivyo, akakanusha juu yao machukizo yaliyopita kwa kukanusha huzuni (juu yao), na yajayo kwa kukanusha hofu (juu yao). Basi watakuwa wameshapata wakipendacho na kikazuilika wanachokichukia juu yao.