Al-Baqara 2:261
البقرةمَّثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنۢبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِى كُلِّ سُنۢبُلَةٍ مِّا۟ئَةُ حَبَّةٍ ۗ وَٱللَّهُ يُضَـٰعِفُ لِمَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ
Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyochipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia moja. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua. [261]
[261] Hakika hali ya wale wanao toa mali yao kwa ajili ya kumt'ii Mwenyezi Mungu na kufanya kheri, na wanapata kwa hivyo thawabu za kuzidia mara nyingi, ni kama hali ya mwenye kuatika punje moja katika ardhi yenye rutuba ikamea mmea wenye mashuke saba, katika kila shuke mna punje mia. Hii ni sura ya wingi wa Mwenyezi Mungu anavyo walipa wanao toa katika dunia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakae. Yeye ni Mwenye wasaa wa fadhila, Mwenye kuwajua wanao stahiki na wasio stahiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa vitu bora zaidi vinavyowanufaisha Waumini ni kutoa katika njia ya Allah Mtukufu. Na mfano wa Waumini wenye kutoa mali yao katika njia ya Allah Mtukufu ni kama mfano wa mbegu iliyopandwa kwenye ardhi nzuri, muda si muda ikatoa mti wenye sehemu saba. Kila sehemu ikatoa suke moja na kila suke likawa na mbegu mia. Na Allah Mtukufu Anamuongezea thawabu anayemtaka, kulingana na kadiri ya Imani aliyonayo yule mtoaji na ikhlasi yake iliyo timamu.Na fadhila za Allah Mtukufu zimeenea, na Yeye, katakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mjuzi wa yule anayestahiki kuzipata, ni Mwenye kujua nia za waja Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net