Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 260

Al-Baqara 2:260

البقرة

وَإِذْ قَالَ إِبْرَٰهِـۧمُ رَبِّ أَرِنِى كَيْفَ تُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ ۖ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِى ۖ قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِّنَ ٱلطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ ٱجْعَلْ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ مِّنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ٱدْعُهُنَّ يَأْتِينَكَ سَعْيًا ۚ وَٱعْلَمْ أَنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Maana

Na Ibrahim aliposema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe vipi unavyofufua wafu. Mwenyezi Mungu akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! Lakini ili moyo wangu utue. Akasema: Basi wachukue wanne katika ndege na uwazoeshe kwako. Kisha weka juu ya kila kilima sehemu katika hao, kisha waite, watakujia mbio. Na ujue kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na alipo sema Ibrahim: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe vipi unavyo fufua wafu. Mwenyezi Mungu akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! Lakini ili moyo wangu utue. Akamwambia: Twaa ndege wane na uwazoeshe kwako, kisha uweke juu ya kila kilima sehemu, kisha wete, watakujia mbio. Na ujue kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, na Mwenye hikima. [260]

[260] Kitaje pia kisa cha Ibrahim alipo sema: Mola wangu Mlezi nionyeshe vipi unahuisha maiti. Mola wake Mlezi akamuuliza Ibrahim, juu ya imani yake kuamini kufufuliwa wafu, ili ajibu Ibrahim kuondoa shaka kabisa katika imani yake. Mwenyezi Mungu akamwambia: Kwani huamini kufufuliwa wafu? Ibrahim akajibu: Mimi naamini, lakini nimetaka ili moyo uzidi kutua. Akasema Mwenyezi Mungu: Basi wachukue ndege wane uwe nao ili uwajue vilivyo. Kisha uwagawe baada ya kuwachinja, na juu ya kila kilima katika vilima vilio jirani weka sehemu yao. Kisha uwete, watakujia mbio, nao ni wahai kama walivyo kuwa. Na jua kuwa Mwenyezi Mungu hashindwi na lolote. Naye ni Mwenye hikima iliyo pita hadi katika kila kitu. Ametaja Al Fakhri Al Razi na wengineo kuwa yapo maoni mengine juu ya tafsiri ya maneno haya matukufu. Nayo ni kuwa Ibrahim hakuwachinja wale ndege, wala hakuamrishwa kuwachinja. Bali aliamrishwa awakusanye kwa kuwazoesha kukaa naye. Kisha akawagawa akaweka juu ya kila kilima ndege mmoja. Kisha akawaita wakamjia. Na hii ni namna Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyo umba, ni kwa amri yake ya "Kuwa" basi huwa, kama alivyo waita wakaja

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Kumbuka, ewe Mtume, maombi ya Ibrãhîm kwa Mola wake Amuoneshe namna ya Ufufuzi. Allah Mtukufu Alimwambia, «Kwani huamini?» Akasema, «La! Nakuamini. Lakini nataka hilo ili nipate yakini zaidi juu ya yakini niliyonayo.» Akasema, «Chukua ndege wanne, uwe nao, uwachinje na uwakatekate kisha weka sehemu ya hao ndege juu ya kila jabali. Kisha waite, watakujia kwa haraka.» Ibrãhîm, amani imshukie, Akawaita. Papo hapo kila sehemu ikarudi mahali pake, na papo hapo wakamjia kwa haraka. Na ujue kuwa Allah Mtukufu ni Mshindi, hakuna kimshindacho, ni Mwenye hekima katika maneno Yake, vitendo Vyake, sheria Yake na makadirio Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net