Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 263

Al-Baqara 2:263

البقرة

قَوْلٌ مَّعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيْرٌ مِّن صَدَقَةٍ يَتْبَعُهَآ أَذًى ۗ وَٱللَّهُ غَنِىٌّ حَلِيمٌ

Maana

Kauli njema na msamaha ni bora kuliko sadaka inayofuatwa na maudhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosheleza, Mstahamilivu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadaka inayo fuatiliwa na maudhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha na Mpole. [263]

[263] Kauli ya kupoza nyoyo na ya kumsitiri hali fakiri usimwambie mwenginewe ni bora kuliko kumpa na baadae ukafuatizia maudhi kwa maneno au vitendo. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la si mwenye kuhitaji watu watoe na huku wanawaudhi mafakiri. Na Yeye anawawezesha mafakiri kupata riziki njema. Wala hafanyi haraka kumuadhibu asiye toa kwa matarajio huenda akaongoka akatoa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Maneno mazuri kujibiwa muombaji na kusamehe utiriri wake katika kuomba, ni bora kuliko sadaka inayofuatiwa na kero na ubaya kutoka kwa mtoaji sadaka. Na Allah Mtukufu ni Mkwasi, Hana haja ya sadaka za waja, ni Mpole Hana haraka nao ya kuwatesa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net