Al-Baqara 2:243
البقرةأَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ خَرَجُوا۟ مِن دِيَـٰرِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ ٱلْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ ٱللَّهُ مُوتُوا۟ ثُمَّ أَحْيَـٰهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ
Je, hukuwaona wale waliotoka katika maboma yao kwa maelfu kwa kuogopa mauti? Na Mwenyezi Mungu akawaambia: "Kufeni!" Kisha akawahuisha. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hukuwaona wale walio toka majumbani kwao kwa maelfu kwa kuogopa mauti? Mwenyezi Mungu akawaambia: Kufeni! Kisha akawahauisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru. [243]
[243] Zingatia, ewe Nabii, hichi kisa cha ajabu, na ukijue! Hao watu walitoka wakaacha majumba yao ati wanakimbia Jihadi kwa kuogopa kufa, na hali wao ni maelfu kwa maelfu. Mwenyezi Mungu akawahukumia kifo na udhalili kutokana na maadui zao. Walipo bakia walio bakia wakasimama kupigana Jihadi, Mwenyezi Mungu aliwapa uhai kwa kuwapa nguvu. Hakika uhai huu wenye nguvu ulio kuwa baada ya madhila umekuja kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, na unastahiki shukrani. Lakini wengi wa watu hawashukuru.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hujui, ewe Mtume, kisa cha waliokimbia kutoka ardhi yao na nyumba zao, wakiwa ni maelfu mengi, wakiogopa kufa kwa sababu ya janga la ugonjwa hatari au vita, Allah Mtukufu Akawaambia, «Kufeni», wakafa, papo hapo, kwa mara moja, ikiwa ni adhabu kwao kwa kukimbia kadari ya Allah Mtukufu, kisha Allah Mtukufu Akawahuisha baada ya muda kupita, ili waukamilishe muda wa uhai wao, na ili wapate kuwaidhika na kutubia? Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye fadhila kubwa kwa watu, kwa neema zake nyingi, lakini watu wengi hawazishukuru fadhila za Allah Mtukufu zilio kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net