Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 243

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ خَرَجُوا۟ مِن دِيَـٰرِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ ٱلْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ ٱللَّهُ مُوتُوا۟ ثُمَّ أَحْيَـٰهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ 243

{243} Yani, je, haukukisikia kisa hiki cha ajabu kilichowatokea wale waliokuwa kabla yenu miongoni mwa Wana wa Israili. Wakati ugonjwa ulipofika katika makazi yao, kwa hivyo wakatoka kwa wingi huu wakiyakimbia mauti. Lakini kukumbia huko hakukuwaokoa, wala hakukuwasaidia kutokana na kuingia katika yale waliyokuwa wakiyatahadhari. Basi akawafanyia kinyume cha makusudio yao, na Mwenyezi Mungu akawafisha hadi mwisho wao. Kisha akawafanyia hisani. Na akawahuisha ima kwa dua ya Nabii kama walivyosema wengi wa wafasiri; na ima kwa lisilokuwa hilo. Lakini hilo ni kwa sababu ya fadhila zake na hisani yake. Naye haijaacha fadhila yake kuwa juu ya watu. Na hilo linawalazimu kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu kwa kuzikubali na kuzitumia katika radhi za Mwenyezi Mungu. Na pamoja na hayo, watu wengi wamepuuza katika wajibu wa kushukuru. Na katika kisa hiki kuna somo kwamba Yeye ana uwezo juu ya kila kitu. Na hiyo ni dalili inayoonekana ya ufufuo. Kwa maana kisa hiki kinajulikana, na kusimuliwa kusimuliwa kusikokuwa na shaka yoyote kwa Wana wa Israili na wale wanaohusiana nao. Na kwa sababu hii ndiyo Mola Mtukufu akakileta kwa mtindo wa amri ambayo inajulikana vizuri miongoni mwa wale walioongeleshwa. Na inawezekana kwamba ni wale waliotoka katika maboma yao kwa sababu ya kuhofia maadui na woga wa kukutana nao. Na hili linaungwa mkono na ukweli kwamba Mwenyezi Mungu alitaja baada ya hapo amri ya kupigana vita. Na akajulisha kuhusu Wana wa Israili kwamba walikuwa wametolewa katika maboma yao na watoto wao. Na kwa uwezekano huu muwili, ndani yake kuna himizo la kufanya jihadi na onyo dhidi ya kukaa na kuiacha. Na kwamba hayo hayafai kitu kutokana na mauti, "Sema: Hata mngelikuwa katika nyumba zenu, basi wangelitoka wale walioandikiwa kuuawa, wakaenda hadi mahali pao pa kufia."