Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَلِلْمُطَلَّقَـٰتِ مَتَـٰعٌۢ بِٱلْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى ٱلْمُتَّقِينَ 241 كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ 242
{241 - 242} Alipoeleza katika Aya iliyotangulia kuwaliwaza wanawake walioachwa kwa sababu ya mauti; akataja hapa kwamba, kila mwanamke aliyetalikiwa ana haki kwa mumewe kumpa cha kumliwaza. Na kumpa kinacholingana na hali yake na hali ya mkewe, na kwamba ni haki waifanyayo wachamungu peke yake. Kwa hivyo, ni miongoni mwa sifa za uchamungu za lazima au za kupendekezwa. Basi ikiwa mwanamke huyo hakubainishiwa mahari maalumu, na akamtaliki kabla ya kuingiliana naye, basi imeshatangulia kuwa inamlazimu mahari kulingana na uwezo wepesi wake na uzito wake. Na kama ameshabainishiwa, basi maliwazo yake yatakuwa nusu ya hicho kilichotajwa. Na akiwa aliingiliwa, basi inapendekezwa kumliwaza kulingana na kauli ya wanachuoni. Na miongoni mwa wanachuoni, kuna wale walioliwajibisha hilo kwa tumia ushahidi wa kauli yake; "ni haki juu ya wachamungu." Na hali ya asili ya haki ni kuwa ni wajibu, hasa na imeifungamanishwa na wachamungu. Na hali ya asili ya uchamungu ni uwajibu. Na Mola Mtukufu alipozibainisha hukumu hizi tukufu kati ya wanandoa wawili, akazisifu hukumu zake. Na kuzibainisha kwake, na kuziweka kwake waziwazi, na kukubaliana kwake na akili zilizo timamu. Na kwamba makusudio ya kuzibainisha kwa waja wake ni kwamba waelewe kutoka kwake yale aliyoyaeleza. Kwa hivyo, wanazielewa kwa kuzihifadhi, na kuzifahamu, na kuzitendea kazi. Kwani, hayo ndiyo katika ukamilifu wa kuzielewa.